Product Category: eBooks

Mahinda Matano

Mahinda Matano alikuwa mwepesi wa kuelewa mambo. Alikuwa mwerevu, mwenye akili timamu na heshima zake za kipekee. Mwalimu wake, Bi Pendo, alimpongeza sana darasani kwa werevu wake kila alipofunza darasani. Watoto kama hao huwa ni kielelezo chema darasani kwa kuwaongoza wenzao ama kuwaelekeza kwa njia inayofana. Darasa lisilo na mwanafunzi sampuli hiyo hukosa mashindano yanayoibua mshindi aliyewapiku
wengine wote. Kila siku, Bi Pendo alisema kuwa, chanda chema huvikwa pete na wanafunzi walielewa maana ya methali hiyo. Walipoufanya mtihani, Mahinda Matano alijitahidi sana kwa uwezo wake wote…