Mahinda Matano

Kshs 250.00

Mahinda Matano alikuwa mwepesi wa kuelewa mambo. Alikuwa mwerevu, mwenye akili timamu na heshima zake za kipekee. Mwalimu…

Categorized in
Quantity
Tagged in ,

Alikuwa mcheshi na mtoto aliyependa mbwembwe za kila aina. Mwalimu wake alimpenda na alijizatiti kuzibadilisha tabia zake zilizoathiri hali yake ya masomo. Mahinda Matano ni mtoto wa shule mtundu na aiyesikia la mwadhini wala la mteka maji msikitini. Anapokuwa darasani huwatumbuiza wanafunzi wenzake. Akiwa nyumbani hufanya vituko na sarakasi ambazo huwaudhi wazazi wake.  Hadithi inakamilika Mahinda akiwa kilema, jambo ambalo linasababishwa na jitihada zake za kukaidi amri za wazazi.

Mahinda Matano ni novela iliyoandikwa kwa ustadi kwa kutumia misamiati inayotumika na mwanafunzi wa shule ya msingi. Aidha ni hadithi yenye mafunzo kwa mwanafunzi na onyo dhidi ya kukaidi nasaha za wakuu. Mwandishi pia ametumia ushairi katika novela hii.